Interviews On the Bench

Three students; Will Iha, Leone Oteba and Festus Kinuthia from the media club did an interview on two teachers; Bw. Evans Mosoti and Mr. Justus Makokha.

Interview with Bw. Evans Mosoti - Will Iha (F2 &) na Leon Oteba (F2 A)
sw. Ni nini ilikuhimiza kuwa
mwalimu?
jb. Sikudhani ningekuwa
mwalimu. Katika familia yetu
mimi ndiye kifungua mimba.
Wanuna wangu walikuwa
wakiniuliza kuhusu masuala
mengi kama kuendesha
baiskeli na pia mambo ya
kimasomo. Hii ilinifanya
kuona kama nina kipawa cha
uongozi na kuona kama
ningekuwa mwalimu bora.

sw. Umefunza shule gani
kabla ya kujiunga na
Strathmore?
jb. Baada ya kuhitimu chuo
kikuu nilianzia taaluma yangu
ya kiualimu Kadino Otunga,
kisha nikajiunga na shule ya
Nova Pioneer na hatimaye kuja
hapa Strathmore.

sw. Nini ilikufanya uje
Strathmore?
jb. Kila mtu, katika taaluma
yoyote huazimia kufika kilele
cha taaluma yake. Strathmore
ni shule tajika nchini. Kwangu
niliona Strathmore kuwa
kilele.

sw. Unafunza madarasa yapi
na somo gani?
jb. Nilikuwa nafaa kufunza
Kidato cha Kwanza na cha pili
lakini Kidato cha tatu pia
hawakuwa na mwalimu,
nikaichukua juhudi ya
kufunza kidato cha pili na cha
tatu. Isitoshe, kama walimu
wa Kiswahili tumekubaliana
kuja pamoja kuwasaidia
Kidato cha nne katika marudio
yao.

sw.Kama mwalimu
unatarajia nini kutoka kwa
wanafunzi wako?
jb. Wanafunzi ambao
wanajituma na wanafunzi
wanaotia bidii katika kazi yao.

sw. Kama mwalimu wa
Kiswahili unaazimia nini
na wanafunzi wako?
jb. Kwanza kabisa, matokeo
bora. Hii ndio ya muhimu
kabisa.
Singependa mwanafunzi wangu kukosa
kujiunga na chuo kikuu kwa
sababu ya kuanguka somo
moja kama Kiswahili.
Pili, ningependa Kiswahili
kuwa lugha yao ya kuongea.
Watu wengi siku hizi hudhani
kuwa Kiswahili ni lugha ya
watu wa kiwango cha chini.
Ningependa kubadililisha
mtazamo huo hasi.

sw. Tangu ujiunge na shule
ya Strathmore, umependa
nini?
jb. Nimependa mambo mengi.
Kwanza, ni mazingira ya
ufanisi mkubwa, unapoingia
shule hii kitu cha kwanza
unachoona ni tuzo ainati, si
michezo tu bali tuzo za
masomo pia. Isitoshe jinsi
wanavyojaribu kuwafunza
wanafunzi mambo ya kidini.
Kama unavyoona kuna kanisa
shuleni na pia hufunzwa kama
somo darasani.

sw. Unapenda kufanya nini
kando na kufunza?
jb. Aghalabu mimi hupenda
kuogelea na kucheza kandanda.
Asante sana Mwalimu!

Evans Mosoti

Interview with Mr. Justus Makokha - Festus Kinuthia (F2&)
Q. How do you find Strathmore?
A. It is a very good school as I have noticed in my stay so far. The atmosphere is very welcoming. The students are
very good and disciplined. The staff is very welcoming too and are great to work with. The environment is conducive for learning and working.
Q. What schools did you 
teach in before coming to Strathmore?
A. 

  • Alliance Girls High School
  • Parklands Girls High school
  • Ngara Girls High School
Q. How are these schools
compared to Strathmore?
A. I take it as a challenge as this is my first time to teach boys. Each school has its own culture. I find Strathmore to
have a very nice culture that other schools should develop. The program in Strathmore is not rigid but rather flexible to the ongoing activities. There is not much pressure on the students especially candidates as the students have freedom to do the right thing. The school also highly values academics as well as sports. Strathmore has a student-driven program that works on discipline as a key thing.
Q. What is your favourite thing about Strathmore?
A. The freedom of students and that they are self-driven as I mentioned before. Students are also willing to learn.

Q. So, what do you do/teach here in Strathmore? 
A. I teach Biology in Form 1 and Form 3. I also teach Geography in Form 1. I am the patron of the French club.
Q. Why did you join Strathmore?
A. I wanted to gain more experience as I mentioned earlier. I have also known it for quite some time since I use the
route neighbouring the school a lot of times. I, as a Catholic, have also heard of Opus Dei. I also take it as a challenge to better my teaching skills for the future.

Q. What is your take on the detention system since the former schools you taught in used corporal punishment?
A. I guess it also depends on the time factor since a punishment like telling a boy to cut grass with a blade will take
a lot of time and this is a day school where school ends at 3:30pm. Detention is an appropriate means of punishing a student since they get to see the sense of the punishment. They also cover up for the time they lost doing their mistake by reading.

Q. Lastly, how do you find the staff in Strathmore?
A. The staff is very welcoming and willing to help. They are an interactive and are willing to help, all the way from the
workers to the principal.

Justus Makokha

Support our bursary fund!